Home Sports GAMONDI AJA NA MKWARA HUU KWA MASTAA WA CAF

GAMONDI AJA NA MKWARA HUU KWA MASTAA WA CAF

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina amewapongeza wachezaji wake kufuatia kufuzu katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akitoa angalizo kwa kuwaambia wana kazi kubwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika hatua hiyo.

Gamondi ametoa kauli hiyo baada ya Yanga kuvunja rekodi ya kufuzu hatua hiyo baada ya miaka 25 kufuatia ushindi wa juzi Jumapili dhidi ya Al Marrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0 ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Rwanda, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kabla ya ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na Clement Mzize.

 Gamondi amesema kuwa alifurahishwa na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wao na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi.

Amesema wachezaji wamecheza vizuri licha ya kutengeneza nafasi za wazi wakafanikiwa kupata moja na kutumia vizuri na kuwapeleka katika hatua ya makundi.

“Sasa ni muda wa kuangalia mechi zilizopo mbele yetu, tunafanya maandalizi hatua kwa hatua mechi kwa mechi, kabla ya kufikiria hatua inayofuata ya michuano ya kimataifa ingawa kwa sasa  tunaangalia mechi yetu ya mbele ambayo ni ligi.

“Najua ukubwa na ugumu wa makundi ya Ligi ya mabingwa kwa sababu zinashiriki timu bora sasa lazima kila mchezaji anatambua nini ambacho tunahitaji kufanya ili tuweze kufanya vizuri kwa sababu hatuwezi kubweteka kwa kuwa tayari tumeshafika katika hatua hii maana nguvu na mikakati inatakiwa kuanzia sasa kwenda mbele,” amesema Gamondi.

Previous articleMAOKOTO YA SPORTPESA YANAWATOA WENGI, MKWANJA NA SIMU
Next articleSIMBA IMETUBEBA TUIPONGEZE NA SI KUIBEZA, LAKINI UKWELI USEMWA