KWENYE mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba 1-1 Power Dynamow, Mzamiru alikomba dakika 58 nafasi yake ikachukuliwa na Willy Onana ambaye ni kiungo mkabaji.
Akiwa benchi Simba ilipata bao dakika ya 69 muda mfupi baada ya kiungo huyo mkabaji kutoka.
Alipotazama wapinzani wao wanashambulia kwa kasi hakuna kiungo mkabaji wa asili, akitazama benchi yupo mkata umeme Sadio Kanoute akimtazama Robertinho anapanga mipango kazi mingine.
Alisikika akimwambia kocha muingize Kanoute akarudi akakaa, mara ya pili akarudi akamwambia Kanoute aiingie tutafungwa.
Mara ya tatu alionekana akimfuata Oliveira tena, hapo mipango ikabadilika Kanoute anaitwa.
Mzamiru akanyanyuka tena akionekana akimwambia Kanoute fanya haraka uiingie.
Kanoute akamaliza kete ya mwisho dakika ya 74 kutembeza mikato ya kimyakimya.