UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Al Merrekh Uwanja wa Azam Complex wapo tayari na maandalizi yanaendelea.
Siku hiyo ya Septemba 30 imepewa jina la Key Day ikiwa ni siku ya Aziz KI kiungo mshambuliaji wa Yanga.
Huo ni mchezo ambao utaamua mshindi atakayetinga hatua ya makundi ambapo kwenye mchezo wa kwanza Yanga iliambulia ushindi wa mabao 0-2 na watupiaji wakiwa ni Kennedy Musonda na Clement Mzize.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ameweka wazi kuwa mashabiki wa Yanga wanaipenda timu yao na wapo tayari kuishuhudia timu hiyo ikipambana kimataifa.
“Ukitaka kujua wana Yanga wana ugwadu na huu mchezo, tayari baadhi yao wameshaingia kwenye mfumo kuangalia tiketi, Tayari baadhi ya mashabiki wameshanunua tiketi kupitia mfumo kabla ya sisi kutangaza mfumo hadharani.
“Sisi sio Klabu namba tatu kwa ubora wa Afrika kwa bahati mbaya, ni lazima tuonyeshe hilo kwa kutinga hatua ya makundi. Hivyo hizi tiketi zinaweza kuisha mapema mno kama shabiki hutanunua tiketi mapema
“Kama una chumba chako kifunge, njoo na funguo Azam Complex itakuwa ni Aziz KI day.
“Kuhusu viingilio mzunguko ni shilingi elfu kumi, VIP B 20,000 na VIP A 50,000,” amesema Kamwe.
Ni Jumamosi ya Septemba 30 mchezo huo wa kimataifa unatarajiwa kuchezwa.