YANGA 1-0 KMC, LIGI KUU BARA

MCHEZO wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 Yanga inaucheza leo Agosti 23 dhidi ya KMC.

Dakika 45 za mwanzo zimemeguka huku Yanga kupitia kwa Dickson Job ambaye ni beki amepachika bao la kuongoza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

Ni dakika ya 16 Job wa Yanga mwenye tuzo ya beki bora msimu wa 2022/23 alifungua akaunti hiyo ya mabao.

KMC wanacheza kwa kujilinda kwenye mchezo wa leo wakiwa imara eneo la ulinzi na lile la kiungo likiwa linapata tabu kuifuata ngome ya Yanga.