KOCHA NAMUNGO ASHUSHA PRESHA

KOCHA Mkuu wa Namungo, Cedrick Kaze amesema kuwa watazidi kuwa imara taratibu kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya kwenye mechi zao zote za ligi.

Timu ya Namungo ilianza kwa kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya JKT Tanzania kwa kufungwa bao 1-0 na mchezo wa pili ilipata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC.

Kaze amebainisha kuwa kuna ushindani mkubwa ndani ya ligi jambo linalowafanya wazidi kujiimaraisha kila wakati.

“Kuwa bora ni mchakato ambao unafanyika na unahitaji muda hilo ni jambo ambalo tunalihitaji kwa namna hali ilivyo kila siku kunakuwa na mabadiliko kwa kuwa makosa tunayafanyia kazi.

“Mchezo wa kwanza kuna mazuri tulifanya na mabaya tuliyokosea hayo yote ni muhimu kwetu kuyachukua na kufanyia kazi kuwa imara kwenye mechi zinazofuata ligi inaanza nasi tunazidi kupambana kuwa imara,” .

Kabla ya kuibukia Namungo Kaze msimu wa 2022/23 alikuwa na kikosi cha Yanga ambacho kilitwaa ubingwa wa ligi.

Kaze alikuwa msaidizi ndani ya Yanga na kocha mkuu alikuwa ni Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambaye naye amesepa ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.