MOSES Phiri msimu wa 2022/23 alitupia mabao 10 kibindoni na timu ya mwisho kuifunga ilikuwa ni Coastal Union, Tanga.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa nyota huyo ataendelea kuwapa furaha Wanasimba.
Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa fainali wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga anaingia kwenye rekodi ya nyota waliokosa penalti.
Agosti 13 nyota huyo alikosa penalti dhidi ya Yanga baada ya kupiga mpira uliokwenda juu na siku ya pili aliandika utani kuwa alichelewa kutuma picha kwa kuwa bado alikuwa anautafuta mpira aliopiga.
Tayari kwa msimu mpya Moses Phiri ambaye alishuhudia kiatu cha ufungaji bora kikiwa mikononi mwa Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibanzokiza ambao wote walifunga mabao 17 amefungua akaunti ya mabao kwenye ligi ambayo imeanza kwa kasi.
Bao la kwanza ndani ya ligi msimu wa 2023/24 kawatungua Dodoma Jiji, kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Ahmed amesema, “Hakufunga muda mrefu Moses Phiri lakini amerejea taratibu nina amini kwamba atafanya kazi vizuri kwa ajili ya kuwapa furaha Wanasimba,”.