TUMEONA namna Ligi Kuu Tanzania Bara ilivyoanza kwa kasi huku kila timu ikipambana kuonyesha uwezo wake ndani ya uwanja katika kutafuta ushindi na hii inaonyesha maandalizi yalikuwa bora.
Pongezi kubwa kwa wachezaji ambao wameanza kuonyesha uwezo wao na hili linapaswa kuwa endelevu na sio kwenye mechi za mwanzo kisha mechi zinazofuatwa ikawa tofauti.
Timu zote ni muhimu kufanya maandalizi mazuri sio Simba, Yanga, Azam FC ama Singida Fountain Gate ambazo hizi zinawakilisha Tanzania anga la kimataifa.
Hakuna ambaye anapenda kuona timu yake ikipoteza hivyo muhimu ni kuendelea kuwa kwenye ubora kwa kila mechi bila kubagua.
Tayari pia kuna timu ambazo zina kazi kwenye mechi za kimataifa huku pia ni muhimu kutafuta matokeo ili kuendelea kuwapa furaha mashabiki.
Mashindano yote ni muhimu wachezaji kuzingatia kufanya vizuri hakuna kingine ambacho kinahitajika. Muda wa maandalizi uliokuwa kwa timu zote sasa umekwisha ni muda wa kurejea kazini.
Kazi ni moja kutimiza majukumu kwa umakini kwa kuwa kila timu inahitaji kufanya vizuri kwenye mechi ambazo inacheza na ushindani ni mkubwa.
Wale ambao wanadhani msimu huu utakuwa ni mwepesi wanapaswa kubadili mawazo hayo na kuamini kwamba ushindani utakuwa mkubwa na kila mmoja atakuwa na malengo yake.
Kitu muhimu ni kuanza kutimiza malengo ya timu kisha mtu binafsi baadaye hilo litakuwa kubwa na litaongeza ushindani zaidi.
Iwe ni mechi za ligi ama kwenye anga za kimataifa bado kinachohitajika ni ushirikiano pamoja na nidhamu kwa wachezaji.
Muda hautoshi lakini unakwenda kasi kutokana na mambo kuwa kwenye ratiba ambazo lazima zikamilike kwa wakati.
Benchi la ufundi, wachezaji, viongozi na mashabiki ni muda wa kushikamana kwenye kila hali bila kubagua mazingira mazuri yanakuwa yenu kisha yakiwa mabaya kila mmoja anamtafuta mchawi.
Umoja ni nguvu itakuwa ajabu wale wenye nguvu wasipokuwa na umoja kwa wakati huu mpaka mwisho wa msimu hapo kutakuwa na anguko ambalo linakaribishwa na wahusika.
Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya imataifa na maandalizi yawe mazuri ili kupata matokeo chanya.
ReplyForward |