Home Sports JEMBE JIPYA LAANZA KAZI MSIMBAZI

JEMBE JIPYA LAANZA KAZI MSIMBAZI

WAKIWA kwenye milima ya Uluguru, Morogoro wachezaji wa Simba wameungana na kipa mpya Ayoub Lakred.

Kipa huyo ni ingizo jipya ndani ya Simba ambapo anakuwa ni kipa wa kimataifa yeye ni raia wa Morocco na watani zao wa jadi Yanga wana kipa raia wa Mali, mdaka mishale Djigui Diarra.

Agosti 15 ilikuwa ni siku yake ya kwanza kuanza mazoezi na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Robert Oliviera.

Agosti 17 Simba inatararajiwa kutupa kete ya kwanza katika Ligi Kuu Bara utakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Yanga ni mabingwa watetezi wa ligi na kete yao ya kwanza inatarajiwa kuwa Agosti 23 dhidi ya KMC.

Ikumbukwe kwamba Simba imetoka kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga kwenye fainali iliyochezwa Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.

Anaungana na makipa wengine ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na Ally Salim pamoja na Hussein Abel ambaye huyu alikuwa ndani ya KMC kipa namba moja Aishi Manula bado hajawa fiti.

Previous articleCHUMA HIKI KINAKUJA SIMBA, YAO, MAXI WAMPA MZUKA GAMONDI
Next articleAZAM FC WATEMBEZA MKWARA HUU, WANA JAMBO LAO