SIMBA WAMESHINDA DHIDI YA TIMU ILIYOONYESHA UBORA

USHINDI wa Ngao ya Jamii ambao wameupata Simba dhidi ya Yanga ni bahati ya mtende kutokana na kiwango cha chini kilichoonyeshwa na wachezaji wa Simba.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ulikuwa unasoma Yanga 0-0 Simba na kupelekea mshindi apatikane kwa penalti.

Katika Ngao ya Jamii kwenye mchezo wa fainali Agosti 13 ni ushindi wa penalti 1-3 Simba walipata dhidi ya Yanga.

Ndani ya dakika 90 uwanjani Yanga walikuwa bora walikosa umakini katika kumalizia nafasi.

Shukrani kwa Ally Salim kipa namba tatu wa Simba ambaye aliokoa penalti tatu.

Lakini kwenye penalti hizo tatu kuna moja aliotea katika kuokoa kwa kuwa alitoka mapema kabla ya mpigaji wa Yanga hajakamilisha pigo la penalti.

Ushindi wa Simba wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Mkwakwani Tanga ni dhidi ya timu iliyoonyesha ubora wa hali ya juu ambayo ni Yanga katika mchezo huku wao wakibebwa na zali la penalti.

Benchi la ufundi la Simba ni muhimu kufanyia kazi makosa ambayo yametokea kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii kuelekea kwenye ligi ambapo huko ni msako wa pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba Yanga na Simba zina kazi ya kuikilisha Tanzania kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa huku Azam FC na Singida Fountain Gate hawa ikiwa ni kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Imeandikwa na Dizo Click.