MPIRA SIO VITA MUHIMU KULINDANA WACHEZAJI

MASHABIKI furaha yao ni kuona wachezaji wakicheza kwa umakini na kuipa ushindi timu yao ambayo wanaishangilia. Ipo hivyo hata kwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenyewe wanapokuwa ndani ya uwanja.

Mashabiki wa Singida Fountain Gate wanapenda kuona timu ikipata matokeo mazuri hata wale wa Kagera Sugar nao pia wanapenda kupata matokeo mazuri.

Miongoni mwa vitu ambavyo huwa vinawapa wakati mgumu makocha katika kufanya mabadiliko ya lazima hasa pale mchezaji anapoumia akiwa kwenye mpango kazi wa kutimiza majukumu yake.

Kuna umuhimu wa wachezaji kuendelea kuongeza umakini kwenye kila mchezo ambao wanacheza, hili litawapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao pamoja na kuwalinda wachezaji wanaokuwa uwanjani kutimiza majukumu yao.

Ngao ya Jamii ni ishara kuwa ligi inakwenda kuanza na kila mchezaji ni muhimu kuongeza umakini ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

Tumeanza kushuhudia wachezaji wakitumia nguvu kubwa katika mechi za ushindani, wsio kila mahali painahitaji nguvu kubwa katika kutimiza majukumu uwanjani hilo lipo wazi licha ya kwamba mpira ni mchezo unaohusisha matumizi ya nguvu nyingi pamoja na akili pia.

Itapendeza ikiwa wale wachezaji ambao wanaotumia nguvu nyingi kujifunza upya namna ya kuwakabili wapinzani kwa kuwa hakuna matokeo mazuri kwenye kumuumiza mchezaji.

Sio wachezaji wa Yanga, Azam FC ama Geita Gold hii ni mpaka kwenye Ligi ya Wanawake ni muhimu wachezaji kuongeza umakini kwenye matumizi ya nguvu hasa katika maeneo ambayo hayana ulazima.

Kila kitu kinawezekana ikiwa wachezaji watakuwa makini kwenye kukamilisha majukumu yao, ni muhimu kulindana ili kuepusha maumivu yasiyo ya lazima na mabadiliko yasiyo ya lazima kwa kuwa mpira sio vita ni mbinu.

Sio Simba, Yanga wala Azam FC ni muhimu kuwa makini kwenye kutimiza majukumu hata Namungo pia muda wa kazi ni sasa.

Kila kitu kinawezekana na wachezaji wakaendelea na maisha kama kawaida bila kuwa na maumivu ambayo hayana ulazima.