KIKOSI cha Yanga kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii nusu fainali ya kwanza.
Yanga inakuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya fainali ya Ngao ya Jamii ikiwa ni mara ya kwanza kuanza kushirikisha timu nne.
Pia ni mchezo wa kwanza kwa Gamondi kwenye mechi za ushindani baada ya kuibuka Yanga akirithi mikoba ya Nasreddine Nabi.
Dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote mpaka kilipokuja kipindi cha pili.
Aziz KI wa Yanga alianza kumtungua Foba dakika ya 84 kisha dakika nne mbele chuma cha pili kikazamishwa.
Ni Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga huyu alipachika bao dakika ya 88 dakika za jioni kabisa.
Yanga inatinga hatua ya fainali ikimsubiri mshindi Kati ya Simba v Singida Fountain Gate ni Uwanja wa Mkwakwani Tanga