Mashabiki ni muda wenu kujitokeza kwa wingi na kushangilia bila kuchoka pale timu zenu zinapocheza hilo litawaongezea nguvu wachezaji.
Jambo la kuzingatia ni kila mmoja kuwa makini katika kutimiza wajibu wake asiwe sababu ya kuleta maumivu kwa wengine ambao watajitokeza uwanjani.
Nina amini kwamba mashabiki wote wanatambua kwamba mchezo wa mpira ni dakika 90 suala la kubeba matokeo mfukoni muda wake umekwisha.
Itakuwa vizuri kwa kila shabiki kuamini kwamba kitakachoamua matokeo sio aina ya wachezaji waliopo kwenye timu bali dakika 90.
Dakika 90 zimebeba yote kwa kila mmoja kupambana bila kuchoka na wao wakiwa majukwaani wanapaswa kushangilia bila kuchoka kuwapa nguvu wachezaji wao.
Masuala ya ugomvi kabla ya mechi na baada ya mechi hayana nafasi kwenye ulimwengu wa mpira hivyo ni jambo la kuzingatia kuwa makini na kutimiza majukumu bila kuleta fujo.
Wachezaji mbinu ambazo mmepewa na benchi la ufundi ni wakati wake sasa kuendelea kutumika katika kutafuta ushindi hivyo tu basi.
Ikitokea ushindi ukapatikana furaha itakuwa kwenu na ushindi ukikosekana bado maisha lazima yaendelee kwa kuwa huu ni mwanzo wa msimu makosa yatafanyiwa kazi.
Mwanzo mzuri ni kivutio pia kwa wadhamini kama ambavyo kampuni ya SportPesa imekuwa ikiwekeza nguvu zake kwenye michezo na masuala ya kurejesha kwa jamii.
Waamuzi jukumu lenu iwe ni kusimamia haki na sharia 17 zifuatwe masuala ya kusema makosa ya kibinadamu hata kwa yale ambayo yanazuilika sio sawa, kila la kheri.
Tayari Singida Fountain Gate wamewasili Tanga kwa maandalizi ya Ngao ya Jamii nina amini timu nyingine zitawasili hivi karibuni.