SIMBA YATUMA UJUMBE KWA MASHABIKI KUONGEZA ULINZI

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Simba amesema Wanasimba wote wenye tiketi za Simba Day wajitahidi kuzilinda.

Agosti 6 2023 ni kilele cha Simba Day ambapo watafanya tamasha lao kwa kutambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi cha Simba msimu wa 2022/23.

Miongoni mwa wachezaji wapya ndani ya Simba ni Fabrice Ngoma ambaye alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga.

Litakuwa tamasha la tatu kwa ukubwa baada ya Yanga kukamilisha Wiki ya Mwananchi ambalo ni la Yanga kisha Singida Fountain Gate wao ni Singida Big Day.

Yanga walifanyia Uwanja wa Mkapa sawa na Simba huku Singida Fountain Gate walifanyia tamasha lao Singida, Uwanja wa Liti.

Simba Day itakuwa ni Agosti 6 Uwanja wa Mkapa huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa rais wa Tanzania Samia Suluhu ikiwa ni taarifa rasmi iliyotolewa na Simba Agosti 4.

Ahmed amesema: “Mwenye tiketi ya Simba Day ajitahidi kuificha yaani usimuamini hata ndugu yako wa karibu anaweza kupita nayo ukamkuta uwanjani,”.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa tiketi zote zimeisha kwenye kila eneo ikiwa ni kuanzia Platinum, mzunguko mpaka VIP.