Home Sports GAMONDI: WACHEZAJI MUHIMU KUONGEZA UMAKINI

GAMONDI: WACHEZAJI MUHIMU KUONGEZA UMAKINI

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wanahitaji kuongeza umakini katika kutimiza majukumu yao yote.

Timu ya Yanga imeweka kambi AVIC Town ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.

Yanga ni mabingwa watetezi baada ya kutwaa taji la ligi msimu wa 2022/23 pia wana kibarua cha kutetea Ngao ya Jamii.

Agosti 3 walicheza mechi mbili za kirafiki ikiwa ni dhidi ya JKU na Friends Rangers ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya.

Miongoni mwa nyota walio katika kikosi cha Yanga ni Aziz KI, Jonas Mkude, Mudhathir Yahya, Farid Mussa.

Kocha huyo amesema ushindani ni mkubwa na wachezaji wanazidi kuimarika taratibu kila siku.

“Wachezaji wanazidi kuwa imara kila siku na hili ni jambo la muhimu. Kila wakati tunahitaji kufanyia kazi yale makosa ili kuwa bora,”.

Yanga inatarajiwa kuanza na Ngao ya Jamii Agosti 9, Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Azam FC.

Previous articleSIMBA TAMBO TUPU MSIMU MPYA, KOCHA ATAMBA
Next articleSIMBA YATUMA UJUMBE KWA MASHABIKI KUONGEZA ULINZI