MCHAKAMCHAKA WA USHINDI UNAANZA SASA

MCHAKAMCHAKA wa maisha ya mpira unazidi kuendelea kasi huku ligi ikiwa mlangoni kuanza. Kwa mipango mipya tunaamini maandalizi ya kila timu yamefanyika kwa wakati.

Licha ya kwamba ilikuwa ni muda mfupi kwa maandalizi ni muhimu kila timu kupambana kutimiza majukumu ambayo yanawahusu hilo ni muhimu kuzingatia.

Tunaona kwamba Namungo imejumuisha wakongwe ndani ya kikosi chao ikiwa ni pamoja na Erasto Nyoni.

Namungo imekuwa na mwendo mzuri kwenye ligi na inaleta ushindani hivyo kuwa na wachezaji wenye uzoefu ikiwa ni pamoja na Shiza Kichuya hii inaongeza kasi kwa msimu mpya.

Sio Namungo tu hata Ihefu pia wamekuwa wakijiimarisha licha ya msimu wa 2022/23 kuanza kwa mwendo wa kususua lakini walikamilisha msimu wakiwa ndani ya 10 bora.

Singida Fountain Gate ambao walikuwa wanaitwa Singida Big Stars nao hawakuwa na jambo dogo hivyo ni mwanzo mwingine unakuja ushindani unahitajika.

Kwa wale ambao wanatambua kuhusu ushindani ndani ya ligi kila msimu umekuwa ukiongezeka na sasa msimu mpya unakuja kwa kila timu kuonyesha uwezo wake.

Usajili ambao umefanyika imani kubwa umefuata vipengele vyote ambavyo ni muhimu kufuata ikiwa ni pamoja na mikataba inayoeleweka kila kipengele.

Wachezaji kazi kubwa kwa msimu ujao ni muhimu kutimiza majukumu kwa wakati hilo litafanya matokeo yapatikane ndani ya dakika 90.

Mashabiki wanapenda kuona ushindi kwenye mechi ambazo zinachezwa na wenye jukumu la kuyatafuta ni wachezaji ambao watakuwa kwenye mchakamchaka wa kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Muhimu kuzingatia hakuna ambaye anakweda uwanja akiwa na lengo la kupoteza hivyo kila timu inahitaji matokeo mazuri ambayo yanapatikana kwa kuzingatia sharia 17 za mpira.

Kila la kheri kwenye mechi za ushindani na wachezaji muhimu kuzingatia maelekezo kutoka kwenye benchi la ufundi na uwezo binafsi kutafuta matokeo.