NTIBANZOKIZA KWENYE REKODI YAKE BONGO

MSIMU wa 2022/23 Saido Ntibanzokiza alipachika mabao 17 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni rekodi yake bora.

Alitwaa tuzo ya kiungo bora msimu wa 2022/23, mfungaji bora licha ya kuwa ni kiungo mshambuliaji na jina lake lilijumuishwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Mshambuliaji Fiston Mayele wa Yanga naye alitupia mabao 17 na alitwaa tuzo ya ufungaji bora.

Ni Saido Ntibanzokiza kiungo wa Simba aliyeibuka hapo akitokea ndani ya Geita Gold.

Raia huyo wa Burundi timu yake ya kwanza kucheza katika ardhi ya Bongo ilikuwa ni Yanga.

Ndani ya Geita Gold alitoa pasi sita za mabao sawa na zile alizotoa ndani ya Simba na kumfanya akamilishe msimu akiwa ametengeneza pasi 12 kibindoni.

Mabao 17 alifunga sawa na Fiston Mayele aliyekuwa Yanga lakini msimu mpya atakuwa kwenye changamoto mpya Klabu ya Pyramids ya Misri.

Mchezo wa mwisho Ntibanzokiza kufunga ilikuwa Uwanja wa Uhuru alipowatungua Coastal Union mabao mawili akifikisha mabao 17 ndani ya ligi.

Alikuwa na timu Uturuki ilipokuwa kambi ya muda na anatarajiwa kuwa kwenye kikosi kitakachotambulishwa Simba Day Agosti 6 watakapocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo.

Tayari kikosi cha Simba kimerejea Bongo baada ya kuweka kambi huko tangu Julai 12 2023.