NYOTA wa zamani wa Arsenal, Julio Baptista amependekeza uhamisho wa mshambuliaji wa Brazil, Neymar unaweza kuwa msingi kwa The Gunners.
Amebainisha kuwa ikiwa Arsenal watampata mshambuliaji huyo watamaliza ukame wao wa taji la Ligi Kuu England.
Arsenal hadi sasa msimu huu wa usajili tayari wametumia takribani pauni 200m kwa kuwavuta Declan Rice, Kai Havertz na Jureien Timber huku pia wakitarajia kumsajili kipa David Raya.
Mwingine anayetajwa kuwa katika hesabu za Arsenal ni Mohammed Kudus .
Baptista anaamini kwamba Arsenal kama watamsajili Neymar anayekipiga PSG basi anaweza kuwasaidia kifikia malengo yao msimu ujao.