KIBEGI CHA SIMBA KISIUZWE, KIPELEKWE MAKUMBUSHO

KIBEGI cha Simba kimefunguliwa juu ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni uzinduzi wa jezi mpya kwa msimu wa 2023/24 ilikuwa Julai 21 2023.

Tumeona namna ambavyo kila mmoja alikuwa akifuatilia kwa namna yake popote alipokuwa kwa kuwa ilikuwa ni habari inayofurahisha.

Utalii wa Tanzania umetengazwa kitaifa na kimataifa wengi wameona na kuendelea kufuatilia zaidi kuhusu mlima Kilimanjaro na vivutio vingine ambavyo vipo hapa.

Nembo ya Visti Tanzania kwenye nembo katika mechi za kimataifa imekuwa ikitumiwa na Simba na huu uwe mwendelezo kwa wale ambao wanafuata.

Kuna mengi ambayo yametokea kupitia kibegi na kuna vingi vitakuja baadae na historia inaandikwa na kila mmoja kuona namna jambo likianza na mwendelezo wake unavyokuwa.

Hakika kila kitengo cha ubunifu kina kazi ya kufikiria ni kipi ambacho kinapaswa kufanywa na kuleta faida sio ndani tu bali hata nje ya nchi.

Kwa namna moja ama nyingine nina amini wapo ambao watakuja Tanzania kufanya utalii kwa ajili ya kibegi cha Simba .

Hii itakuwa bora kama wahusika watafikiria kukipiga mnada kibegi ni sawa ila itapendeza zaidi kikiwekwa makumbusho hiyo itakuwa ni mwendelezo.

Wale ambao watatoka nje ya nchi kuja Tanzania kukiona kibegi watafarijika wakikiona kibegi chenyewe kilichokwea mlima Kilimanjaro kikiwa na uzi mpya wa 2023/23.

Bado fedha ambayo inatafutwa itapatikana na kila mmoja atatimiza kile ambacho alikuwa anafikiria baada ya kukiona kibegi.

Mbali na hilo pia iwe ni mwendelezo kwa wengine kuendeleza ubunifu kwenye uzinduzi sio jezi tu hata matamasha ambayo yanaandaliwa kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji ni muhimu kuwa na ubunifu.

Kupitia ubunifu huo itaongeza nguvu ya ushawishi pamoja na kukubalika kwenye kazi husika ambayo inafanyika.