AZAM WATAJA SABABU KUVUNJIKAMCHEZO MBELE YA WAARABU

HASHEEM Ibwe Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa sababu iliyofanya mchezo wao wa kirafiki kuvunjika katika dakika ya 60 ni kutokana na kutokuwa mchezo wa kiungwana kwa asilimia kubwa.

Timu hiyo imeweka kambi Tunisia ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 na wamekuwa wakicheza mechi za kirafiki kuongeza hali ya kujiamini

Kwenye mchezo uliochezwa Julai 26 wakiwa Tunisia mchezo huo ulikwama kugota mwisho baada ya benchi la ufundi kuwaambia wachezaji watoke nje.

“Ilikuwa mwanzo wapinzani wetu walipata penalti ambayo hatukujua imetokana na nini hivyo mwamuzi aliendelea na maamuzi yake benchi la ufundi likazungumza na mwamuzi akasema atajirekebisha.

“Ilitokea tena mchezaji wetu mwingine Charlse Manyama yeye aliumizwa mkono bado mwamuzi aliendelea na akatoa penalti nyingine kipindi cha pili kisha baadaye akaifuta hivyo benchi la ufundi likaona hakuna utulivu na ni mechi ya kirafiki.

“Utulivu ukiwa hakuna na mwamuzi hayupo kwenye uungwana hapo unakuwa sio mchezo wa kirafiki tukaamua kuondoka na tulikuwa na uwezo wa kurudisha mabao ambayo wametufunga,” amesema Ibwe.

Mchezo huo wa kirafiki Azam FC 1-3 Stade Tunisien ilikuwa huku bao la Azam FC likifungwa na Prince Dube
Dube.