JULAI 23 rasmi kipa Jefferson Luis Szerban de Oliveira alitambulishwa ndani ya Simba na yupo kambini Uturuki akiwa na wachezaji wengine na kufanya chama la Simba kuwa kamili gado.
Ipo wazi kuwa msimu wa 2022/23 Simba walikuwa mashuhuda wa mataji yote yakienda kwa watani zao wajadi Yanga.
Yanga ilitwaa taji la Ngao ya Jamii, Kombe la Azam Sports Federation ubao wa Uwanja wa Mkwakwani kwenye fainali ulisoma Azam FC 0-1 Yanga na pia ilitwaa taji la ligi.
Ikumbukwe kwamba Simba mchezo wake wa ufunguzi kwenye Ngao ya Jamii msimu wa 2023 itakuwa dhidi ya Singida Fountain Gate Tanga, Uwanja wa Mkwakwani baada ya utaratibu kubadilika na msimu huu watacheza kwa mwendo wa mtoano timu nne.
Hivyo Simba imeongeza nguvu kwenye upande wa usajili ambapo mbali na Luis ambaye ni kipa ameungana na nyota wengine wapya ambao ni Willy Onana, Che Malone Fondoh, Aubin Kramo, Fabrice Ngoma.
Pia yupo kiungo Luis Miqussone, David Kameta wengi hupenda kumuita Duchu, Hamiss Abdallah, Hussein Kazi na Shaaban Chilunda hawa kuanzia kwa Duchu ni wazawa.
Julai 12 Simba iliwasiri Uturuki kwa maandalizi ya msimu mpya na Simba Day inatarajiwa kuwa Agosti 6 2023, Uwanja wa Mkapa