Skip to content
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba Charles Ilanfya anatajwa kufikia makubaliano mazuri na Ihefu muda wowote atasaini mkataba mpya na kutangazwa.
Ihefu ya Mbeya ni timu ya kwanza kuifunga Yanga kwenye ligi kwa msimu wa 2022/23.
Ikumbukwe kwamba wakati rekodi ya Ihefu kuifunga Yanga inaandikwa timu ya Yanga ilikuwa imecheza mechi 49 za ushindani kwenye ligi bila kufungwa.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu 2-1 Yanga.
Ilanfya msimu wa 2022/23 alikuwa anacheza Mtibwa Sugar alipokuwa akitimiza majukumu yake kwenye ligi.
Nyota huyo amecheza timu kadhaa kwenye soka la ushindani ikiwa ni pamoja na KMC, Mwadui na Simba.
Mtu wa karibu wa Ilanfya aliyefunga mabao sita kwenye ligi akiwa na Ihefu alisema kuwa mshambuliaji huyo amefikia makubaliano mazuri na Ihefu.
“Mpaka sasa ni sehemu nzuri ambayo wamefikia mchezaji na timu kinachosubiriwa ni kusaini na kutambulishwa hivyo tu basi,” ilieleza taarifa hiyo.
Ilanfya amesema kuwa kuna timu ambazo zimepeleka ofa muda ukifika itafahamika.
“Msimu mpya unakuja ninatambua na changamoto mpya ni muhimu hivyo wakati ukifika itafahamika wapi ambapo nitakuwa,” alisema Ilanfya.