BAADAE kidogo ni nadra sana kufika ila sasa hiyo ipo muda wote hivyo ni muhimu kuifanyia kazi kwa umakini mkubwa.
Muda uliopo kwa sasa kwa Yanga ni kuboresha zaidi ya yale waliyofanya wakati uliopita kwenye Wiki ya Mwananchi ili izidi kuwa ya utofauti.
Maandalizi kwa Yanga tangu awali yameonekana kwenda kulingana na mipango yao katika hilo wanapaswa pongezi.
Ukweli ni kwamba, muda kwa sasa unazidi kusogea na muda wa kuanza ligi upo njiani hivyo kila kitu kinapaswa kwenda kwa mipangilio makini.
Wakati Yanga wakianza na Wiki ya Mwananchi, tunaamini kwamba kuna timu zingine nazo zina mpango wa kufanya utambulisho wao.
Sio vibaya kuweka wazi mipango yao mapema kabla ya ligi kuanza kwa kuwa ni muda uliopo sasa kutimiza kila mmoja majukumu yake.
Hakuna ambaye hapendi kuona kitu cha upekee katika kazi ambayo anafanya na hiyo inaongeza ubora wa kitu ambacho kinatafutwa.
Yote ni sasa na sio baadae kwa kuwa baadae ni ngumu kufika na muda uliopo ni sasa kukamilisha kila kitu ambacho kinahitajika kufanyika kwenye ligi na anga la kimataifa.
Mipango ikianza mapema inapunguza presha ya kufanya vibaya kwenye mechi za ushindani pamoja na kuongeza ushirikiano ndani ya timu.
Ni rahisi wachezaji kuwa timu moja kwa sasa ikiwa maandalizi ya msimu mpya yatatumika kwa umakini na ushirikiano mkubwa.
Hivyo kila la kheri wawakilishi kwenye mashindano ya kimataifa, maandalizi ya Championship bila kusahau Ligi ya Wanawake Tanzania jambo la msingi kuzingatia ni kuanza sasa.