KUJENGA wazo la kuanza nalo mwanzo ni muhimu kwa kuwa litatoa picha kamili ya kile ambacho utakifanyia kazi wakati ujao.
Hilo ni muhimu ikitokea wazo litakuwa la kawaida hata matokeo pia yatakuwa ya kawaida lakini kama wazo litakuwa kubwa ambalo linakuogopesha litaleta matokeo mazuri.
Kila mmoja kwa sasa yupo kwenye mipango ya kujenga timu kwa ajili ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ikiwa ni pamoja na mabingwa watetezi Yanga.
Jambo pekee ambalo linapaswa kufanyiwa kazi ni lile wazo la mwanzo litakalobeba malengo ya timu husika iwe inashiriki ligi, Championship ama Ligi ya Wanawake.
Kwa msimu uliopita mawazo mengi ya timu yalikuwa makubwa lakini yalikwama kutokana na sababu ambazo wahusika wanatambua.
Wapo waliokuwa na malengo ya kutwaa ubingwa na yote haya yalitokana na lile wazo la awali kabla ligi haijaanza hivyo na sasa ni muda wa kutazama upya malengo.
Muda wa kuyaweka wazi malengo kwa ajili ya msimu mpya ni sasa hivyo maandalizi ni muhimu.
Kwa kushindwa kufikia malengo ni muhimu kuangalia upya namna bora itakayoleta matokeo mazuri kwa msimu mpya.
Wale ambao malengo yalitimia ni muda wa kuangalia namna gani wataendelea kuwa imara kwa msimu mpya ambao ushindani haukwepeki.
Kikubwa ni kuwa na mipango makini itakayoleta matokeo mazuri uwanjani baada ya dakika 90 kwenye mechi za ushindani.
Mashabiki ni muda wa kuwa tayari kwa ajili ya msimu mpya kuendelea pale ambapo mliishia msimu uliopita katika kushangilia timu zenu.
Kila kitu kinawezekana kwa kuwa yote yaanzia kwenye mawazo bora ambayo ni muhimu kuyaboresha kila leo.
Azam FC wao ngome yao ipo Tunisia wakiendelea na mipango kwa ajili ya msimu mpya.