SIMBA KAZI INAENDELEA MATIZI KAMA YOTE

WAKIWA Uturuki tayari wameanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa Bongo, Avic Town.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Simba ilipishana na mataji yote iliyokuwa inapambania na kushuhudia watani zao wa jadi Yanga wakitwaa mataji hayo.

Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kikosi cha Simba kinajifua ili kurejea kikiwa imara tayari kwa mashindano.

Oliveira aliweka wazi kuwa anatambua msimu mpya utakuwa na ushindani mkubwa lakini wapo tayari kupata matokeo mazuri.

“Ni msimu ambao utakuwa na ushindani mkubwa lakini tunafanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo chanya nina amini kila kitu kitakuwa sawa,”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini Uturuki ni pamoja na David Kameta, ‘Duchu’, Henock Inonga, Mohamed Hussein, John Bocco na Moses Phiri.