KOCHA MPYA YANGA, KAZE IMEISHA

KALBU ya Yanga imemtambulisha kocha msaidizi ambaye  ni Moussa Ndao raia wa Senegal.

Anaungana na Miguel Angel Gamondi ambaye huyu ni mkuu kwenye benchi la ufundi ndani ya kikosi cha Yanga.

Julai 11 Ndao alitambulishwa rasmi ndani ya Yànga ambao ni mabingwa watetezi.

Anachukua mikoba ya Cedric Kaze ambaye alikuwa akifanya kazi na Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Timu hiyo umeweka kambi Avic Town, Kigamboni kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.