KUTOKA Morogoro izilipo safu za milima Uluguru mpaka Dar ulipo Uwanja wa Mkapa, Uhuru na Chamanzi na mingine yote unayoitambua mwamba Shomari Kapombe bado yupoyupo.
Ni dili la miaka miwili ameongeza ndani ya kikosi cha Simba hivyo atakuwepo mpaka 2025.
Kapombe ni namba moja kwa mabeki wenye pasi nyingi ambazo ni 8 kwa msimu wa 2022/23 hivyo kazi yake itaonekana na mashabiki pamoja na familia yake akiwa na Simba.
Beki huyo hatakuwa peke yake atakuwa na mshikaji wake Mohamed Hussein ambaye ni nahodha msaidizi wote wameongezewa kandarasi ya miaka miwili.