AUBIN Kramo ambaye ni winga ametambulishwa kuwa ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Ni nyota kutoka Klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast anaingia kwenye orodha ya nyota wapya watakaokuwa kwenye kikosi cha Simba.
Huyu ni mchezaji wa pili kutambulishwa baada ya awali kuaza na Willy Onana ambaye naye ni winga aliyekuwa anakipiga Rayon Sports ya Rwanda.
Timu hiyo inajipanga kwa ajili ya msimu ujao na inatarajia kuweka kambi Uturuki kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24.