Skip to content
MSAFARA wa Yanga leo Julai 5 umeanza safari kwa ajili ya kuelekea nchini Malawi.
Timu hiyo imealikwa katika mchezo maalumu wa siku ya Uhuru ikiwa ni miaka 59 ya Uhuu wa Malawi.
Julai 6 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kucheza mchezo maalumu katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru.
Miongoni mwa nyota waliopo katika kikosi ni Dennis Nkane, Joyce Lomalisa pamoja na mastaa wengine kutokà U 20.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa hiyo kwao ni heshima kwa Yanga pamoja na taifa la Tanzania kiujumla.
“Ni heshima kwa Yanga na Tanzania pia kuwa kwenye mualiko huu maalumu hivyo tunakwenda kufanya kazi kwa ajili ya Tanzania,”.