ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA HUYO KAIZER

MKALI wa kutupia kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Ranga Chivaviro ametambulishwa rasmi na kuwa ni mchezaji halali wa klabu ya soka ya Kaizer Chiefs ya nchini humo.

Mshambuliaji huyo kutoka Marumo Gallants iliyoshuka daraja msimu uliopita amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka miwili huku kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Nyota huyo alifunga mabao sita akizidiwa bao moja na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ambaye alifunga mabao 7.

Ranga Chivaviro (30) alihusihwa kutakiwa na Yanga kwa msimu ujao wa soka baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika, kiwango ambacho kiliwavutia mabosi wa timu ya wananchi, Yanga yenye makao yake makuu mitaa Jangwani, jijini Dar.

Aidha, Kupitia ukarasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa klabu hiyo Kaizer Chiefs wamethibitisha kumsajiri mshambuliaji huyo kwa kuandika “Tunapenda kuthibitisha rasmi usajili wa Ranga Piniel Chivaviro kutoka Marumo Gallants.

“Nyota huyo ametia wino kwenye karatasi baada ya kukubaliana na mkataba wa miaka miwili na chaguo la mwaka mmoja. Atavaa jezi maarufu namba 7”