RAIS wa Shirikisho la Mpirawa Miguu Tanzania, (TFF) Wallace Karia amesema shindano la Ngao ya Jamii ambalo linategemea kuhusisha timu 4 ambazo ni Simba, Yanga, Azam na Singida Fountain Gate litafanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Karia amesema: “Kwenye Ngao ya Jamii ambayo msimu huu zitachezwa mechi tatu, mbili za Nusu Fainali na moja ya Fainali, mechi zote zitachezwa Mkwakwani Tanga kwa sababu Uwanja wa Uhuru na Benjamin Mkapa vimefungwa na Uwanja wa Mkwakwani upo karibu na katika utaratibu mzuri,” .
Ikiumbukwe mnamo Agosti 2022 bodi ya Ligi TPLB ilibadili utaratibu wa shindano la Ngao ya Jamii kutoka mfumo wa timu mbili na kuwa timu nne.
Kwa mujibu wa utaratibu mpya unaohusisha shindano la Ngao ya Jamii timu zinazotarajiwa kushiriki shindano hilo kwa msimu wa 2023-24 ni Yanga SC (Mabingwa), Simba SC (Nafasi ya Pili ), Azam FC( Nafasi ya Tatu) na Singida Fountain Gate(Nafasi ya Nne)
HATUA YA NUSU
Simba vs Azam
Yanga vs Singida Fountain Gate
FAINALI
Mshindi wa mchezo wa Simba/Azam dhidi ya mshindi wa Yanga/Singida Fountain Gate.
Pia, ikumbukwe kwamba Yanga ataingia kwenye mchuano huo wa timu 4 akiwa ndiye bingwa mtetezi wa taji hilo baada ya kutwaa taji hilo msimu uliopita.