MWAMBA ANAYETAJWA YANGA KUIBUKIA JKT TANZANIA

INAELEZWA kuwa Hassan Nassoro kiungo mshambuliaji wa Mbeya City yupo kwenye rada za JKT Tanzania kwa ajili ya kuinsa saini yake.

Rasta huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabingwa wa ligi Yanga ambao walikuwa wanahitaji saini yake.

Mbali na Yanga pia Singida Big Stars nao walikuwa wanatajwa kuiwinda saini ya mwamba huyo kwa ajili ya msimu wa 2023/24.

Mbeya City imeshuka daraja itashiriki Championship msimu wa 2023/24 baada ya kuondolewa kwenye mchezo wa mtoano dhidi ya Mashujaa kwa jumla ya mabao 4-1.

Habari zinaeleza kuwa JKT Tanzania wamempa dili kiungo huyo amaye mkataba wake ndani ya Mbeya City umegota mwisho mwishoni mwa msimu hivyo anajiunga akiwa huru.