KIUNGO HUYU APEWA DILI LA MIAKA MIWILI YANGA

MUDA wowote Yanga watatangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wake mchezeshaji, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’. Kiungo huyo alijiunga na Yanga katika msimu uliopita akitokea Azam FC ambayo ilivunja naye mkataba. Yanga imepanga kuiboresha safu hiyo ya kiungo kwa ajili ya msimu ujao ambao wanakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika. Taarifa zinaeleza kuwa Yanga wamefikia…

Read More

SIMBA YAMFUATA MWAMBA HUYU

KLABU ya Simba imerudi tena ndani ya klabu ya Cotton Sports FC ya nchini Cameroon kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa kati Che Fondoh Molane. Beki huyo ni kati ya wachezaji waliokuwa katika mipango ya kusajiliwa na Simba katika msimu huu katika kuiboresha safu ya ulinzi. Simba hivi karibuni ilitangaza kuachana na beki…

Read More

CV YA KOCHA MPYA YANGA IPO NAMNA HII

YANGA SC, imemtangaza Miguel Ángel Gamondi, kuwa kocha mpya wa timu hiyo akichukua mikoba ya Mtunisia, Nasreddine Nabi ambaye waliachana naye hivi karibuni baada ya mkataba wake kufikia tamati. Gamondi raia wa Argentina, anajiunga na Yanga akiwa mzoefu wa kufundisha soka Afrika kwa zaidi ya miaka 20, huku muda wake mwingi akiutumia kufundisha timu za…

Read More

KIPA SIMBA SAFARI YAKE SINGIDA FOUNTAIN GATE

BAADA ya mkataba wake kugota mwisho ndani ya kikosi cha Simba kipa Beno Kakolanya ameziingiza vitani Azam FC na Singida Big Stars ambayo kwa sasa inaitwa Singida Fountain Gate. Ni Singida Fountain Gate yenye maskani yake Singida hii inapewa nafasi kubwa kumnasa. Kipa huyo alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kilichopata ushindi…

Read More

ISHU YA MORRISON KUIBUKIA AZAM IPO HIVI

IMEKUWA ikitajwa kuwa mabosi wa Azam FC wapo kwenye mpango wa kuinasa saini ya Bernard Morrison. BM aliyekuwa kiungo wa Yanga raia wa Ghana kwa sasa yupo huru jambo lililowafanya viongozi wa klabu hiyo kuibuka na kuweka wazi kuwa nyota huyo hayuko kwenye mipango yao. Morrison alitangazwa kutokuwa kwenye mipango ya Yanga kwa msimu ujao…

Read More