LEGEND MKUDE, NYONI THANK YOU HAZIWATOSHI

LEGEND Jonas Mkude anaingia katika orodha ya Thank You huku akinyimwa maua yake.

Amevuja jasho kuipambania nembo ya Simba akiwa ni miongoni mwa nyota waliocheza mechi nyingi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga hili sio jambo dogo ujue.

Kupata nafasi kikosi cha kwanza mbele ya watani wa jadi Yanga katika kikosi cha Simba inaonyesha ukomavu na uwezo ambao upo kwenye miguu yake anahitaji zaidi ya Thank You.

Kuwa na kipindi kigumu na kizuri ñdani ya Simba yote akipita na kuinuka haina maana kwamba mazuri yote yawekwe kando mazima na kugotea kwenye neno Thank You.

Mkataba wake umegota mwisho sawa, mtukutu sawa je kuna mpango mwingine wa kumuaga Legend Mkude?

Zaidi ya miaka 10 kuwa na timu kisha anaagwa kupitia mitandao ya kijamii kwa neno Thank You bado kuna deni na maua yake apewe.

Sio Mkude pekee hata Erasto Nyoni mpigaji bora penalti wa muda wote Simba naye inatosha kukumbuka yote kwa Thank You.Licha ya kuwa shuhuda taji likienda Yanga la ubingwa bado wamevuja jasho hawa miamba.

Beno Kakolanya uwezo wake umegotea benchi kisha Ally Salim kapeta naye maua yake je wapi?

Maamuzi yameshapita lakini hawa wote wanahitaji zaidi ya Thank You kuna wakati Thank You haitoshi.

Wanahitaji zaidi ya Thank You kuagwa kwenye mitandao kwa kazi ambayo wamefanywa hiyo haitawapa kumbukumbu nzuri, maisha ya mpira ni amani na upendo, wapewe maua yao.