NAMUNGO FC imemtambulisha rasmi nyota wa zamani wa Simba, Erasto Nyoni kuwa mali yao kwa msimu wa 2023/24.
Nyoni ni kiraka anayefiti kila eneo ambalo atapangwa kucheza na benchi la ufundi iwe kwenye eneo la ukabaji, ulinzi na ushambuliaji uwezo wake unahamia Namungo.
Uwezo mkubwa ni kutumia mguu ule wa kulia ambao umekuwa ukifanya kazi ya kupiga pasi na kutuliza hatari.
Katika kikosi cha Simba alijenga ngome kwenye eneo la mapigo huru hasa penalti akiwa ni miongoni mwa wale waliofunga katika penalti ya ufunguzi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.
Nyoni amewahi kuitumikia Azam FC kisha kuibukia Simba ambapo Juni 22,2023 alipewa mkono wa asante na mabosi wa Simba kumtakia kila la kheri.
Maisha mapya yanakwenda kuanza Uwanja wa Majaliwa, kila la kheri Nyoni.