WAPEWA MKONO WA ASANTE AZAM FC

KIUNGO wa Azam FC Keneth Muguna ni miongoni mwa nyota ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24.

Raia huyo wa Kenya hajawa na msimu bora ndani ya 2022/23 kutokana na kushindwa kuonyesha makeke yake.

Ni shuhuda wa timu hiyo ikipoteza mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation kwa ubao wa Uwanja wa Mkwakwani kusoma Azam FC 0-1 Yanga.

Pia Rodgers Kola naye ambaye ni mshambuliaji raia wa Zambia naye pia hatakuwa kwenye kikosi hicho.

Mwingine ni Bruce Kangwa ambaye alijiunga na timu hiyo 2016.