MABINGWA wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 Yanga leo Juni 10, 2022 wameandaa paredi la ubingwa wao.
Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Sokoine ukisoma Tanzania Prisons 0-2 Yanga.
Mabao ya Yanga ni mali ya Fiston Mayele mwenye mabao 17 pamoja na Yannick Bangala ambaye naye alitupia bao ugenini.
Baada ya mchezo huo walikabidhiwa taji la msimu wa 2022/23 na miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye sherehe hizo ni pamoja na beki Dickson Job, Kibwana Shomary na Aboutwalib Mshery hawa wote kutoka pande za Morogoro.