VIGONGO VYA LIGI KUU BARA LEO HIVI HAPA

KIGONGO cha 30 kwa timu zote ndani ya Ligi Kuu Bara ni leo Juni 9,2023 mwisho wa ubishi kwenye vita ya ufungaji na zile ambazo zitacheza hatua ya mtoano.

Kesi ya ubingwa imefungwa Yanga ni bingwa kwenye kiatu cha ufungaji bora Fiston Mayele wa Yanga anaongoza akiwa na mabao 16 na Saido Ntibanzokiza wa Simba anafuata akiwa na mabao 15.

Dakika 90 zitaamua kiatu kitakwenda Yanga ama kitakwenda Simba kwa msimu wa 2022/23.

Itakuwa namna hii:-Tanzania Prisons vs Yanga ngoma inapigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Simba dhidi ya Coastal Union ngoma inapigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

Azam FC V Polisi Tanzania inapigwa Azam Complex, Dar.

Namungo FC vs Singida Big Stars
ni Ruangwa Lindi.

Mtibwa Sugar dhidi ya Geita Gold ni Uwanja wa Manungu Complex, Moro.

Ihefu FC dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Highland Estate Mbarali

Ruvu Shooting FC vs Dodoma Jiji FC
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro,

Mbeya City vs KMC Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.