TANZANIA PRISONS YAPOTEZA MBELE YA YANGA

BAADA ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine umesoma Tanzania Prisons 0-2 Yanga.

Kwenye mchezo wa leo wa kufunga msimu wa 2022/23 Nasreddine Nabi kocha wa Yanga alianza na kikosi chote cha kazi ikiwa ni pamoja na Joyce Lomalisa, Djigui Diarra.

Ni bao la Fiston Mayele dakika ya 33 na lile la pili likifungwa na Yannick Bangala dakika ya 90.