HAKUNA KAZI NYEPESI MUHIMU KUJITOA

TAYARI kete ya kwanza imeshachezwa na kila mmoja ameona namna hali ilivyokuwa kwenye mchezo wa fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Leo msafara wa Yanga umeanza safari kueleka Algeria iwe ni safari njema na yenye mafanikio kwenu wawakilishi wa Tanzania kimataifa.

Hakuna ambaye alikuwa amebeba matokeo uwanjani kwenye mchezo wa fainali ile ya kwanza licha ya kwamba kila timu ina nafasi ya kushinda na nina amini ilikuwa hivyo.

Mashabiki wa Yanga wanatambua namna ushindani ulivyokuwa mkubwa kutokana na kazi kubwa iliyopo uwanjani kwenye mechi za ushindani

Kushindwa kupata matokeo kwenye mchezo wa kwanza haina haina maana kwamba kazi imekwisha bado kazi inaendelea kwa kuwa mchezo wa fainali ya pili utatoa picha kamili.

Wawakilishi wa Tanzania, Yanga kwenye anga la kimataifa wanakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya USM Alger katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kila mmoja anatambua namna umuhimu wa kupata ushindi ndani ya uwanja na hapa ni muda wa kwenda kukamilisha hesabu na kuandika rekodi mpya.

Dakika 90 za nyumbani hazikuwa nzuri kwa Yanga kwani walipoteza na mashabiki waliojitokeza waliondoka wakiwa wameinama.

Kushindwa nyumbani iwe ni hasira ya kwenda kwenye mchezo wa pili dhidi ya USM Alger huko ugenini nchini Algeria na muda ni sasa.

Wale wachezaji wenye kazi kubwa kusaka ushindi ni muhimu kuwa kwenye kazi kwa umakini na kupambania ushindi ndani ya dakika 90.

Ugumu upo na kila mmoja anatambua namna Watanzania ambavyo wanapenda kupata ushindi na kushindwa kufanya kazi nzuri kwenye mechi ya pili.

Ni mchezo wa kuandika historia katika kila idara na muda ni huu kufanikisha jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi kila mmoja kuanzia wachezaji pamoja na mashabiki.

Sio kazi nyepesi kwa wachezaji ugenini kwani falsafa ya mpira wa Afrika unajulikana namna mbinu zinavyokuwa kwenye mechi za ugenini.

Kila mmoja wanasema ashinde mechi zake hilo lipo lakini Yanga walifanikiwa kushinda ugenini kwa baadhi ya mechi ambazo walicheza hivyo wana kazi ya kufanya ugenini kutafuta ushindi.

Niwakumbushe wachezaji kuwa matokeo yanapatikana uwanjani na sio kwenye maneno ama ahadi ni kazi kubwa kwenye kutafuta matokeo.

Ikiwa wao walifanikiwa kushinda nyumbani basi ni muda wenu wachezaji kupata ushindi kwenye ardhi ya ugenini katika kusaka ushindi.

Fursa kubwa kwa wachezaji kushinda mchezo wa fainali na kurejea na Kombe la Afrika kwa kila mmoja kuamua kujituma na kufanya kazi ila kuogopa.

Hakuna cha kupoteza kwa sasa kwenye mchezo wa pili ukizingatia wapinzani wanaamini kazi imeisha baada ya mchezo wa kwanza kushinda katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Sio kazi nyepesi kushinda ikiwa mtabeba matokeo mfukoni ni muhimu kujua hakuna kitu kama hicho na kinachotakiwa ni kujituma mwanzo mwisho.

Benchi la ufundi linatambua makosa ambayo yamefanyika hivyo ni muhimu kufanya kazi kubwa kusaka ushindi.