Home Sports HUYU HAPA BOSI MPYA MITAA YA MSIMBAZI

HUYU HAPA BOSI MPYA MITAA YA MSIMBAZI

MKUU wa Programu za Vijana wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa ili kufikia malengo kwenye anga la michezo ni lazima kuwepo na uwekezaji kwa vijana.

Miongoni mwa vijana waliopita ndani ya Simba ni pamoja na Ibrahim Ajibu aliyepata nafasi ya kucheza Yanga, Jonas Mkude, Said Ndemla hawa walikuwa wanatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga nyakati fulani.

Rweyemamu leo Mei 31 ametanagzwa rasmi kuwa mkuu wa program ya vijana ndani ya Simba kwa ajili ya kuona matokeo bora kwenye sekta ya michezo.

Anakuwa bosi mpya kwenye idara ya vijana ndani ya timu hiyo.

Kiongozi huyo amesema:”Mpira hauwezi kuendelea bila kuwa na uwekezaji kwa vijana. Tulishawahi kufanya hii kazi na matunda yake yanajulikana.

” Kuanzia 2008 hadi 2015 tumetoa wachezaji takribani 250. Hakuna timu za ligi hadi madaraja ya chini iliyowahi kukosa wachezaji ambao wamepita kwenye timu ya vijana ya Simba.

“Tunatafuta wachezaji wenye vipaji, wenye uwezo, tunatengeneza ajira na tunapunguza mchakato wa usajili sababu kutafuta kitu ambacho hujawekeza kina gharama yake.

“Kuna kizazi kinapotea kwenye mpira hivyo lazima tuandae kizazi kipya ambacho kitasaidia Simba na Taifa kwa ujumla.”

Previous articleSIMBA KUJA KIVIGINE TENA MASHINDANO YAJAYO
Next articleSEVILLA WASEPA NA TAJI LA SABA LIGI YA EUROPA