INAELEZWA kuwa Chelsea wamefanya mazungumzo juu ya kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon Manuel Ugarte kwa ajili ya kupata saini yake.
Nyota huyo dau lake linatajwa kuwa na kipengele cha kuachiliwa kwa gharama ya Pauni 60.
Mkataba wa Ugarte unamalizika 2026 na Kocha Mkuu wa Sporting Ruben Amorim amekiri itakuwa vigumu kuwabakisha wachezaji kama Ugarte kufuatia kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
PSG pia wana nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 22.
Chelsea wamemteua kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mkuu mpya kwa mkataba wa miaka miwili, huku kukiwa na chaguo la mwaka mmoja zaidi, kuanzia Julai Mosi.