UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ka sasa hali ya kiungo wao Hassan Dilunga ambaye hakuwa fiti kutokana na kupambania afya yake imezidi kutengamaa.
Kwenye ligi Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 na vinara ni Yanga wenye pointi 74.
Yanga wametwaa taji la ligi ikiwa imebakiwa na mechi mbili mkononi.
Dilunga hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa muda mrefu na hata siku ya Simba Day hakutambulishwa na jezi yake hakuna mchezaji ambaye alipewa.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa kwa nyota huyo inasubiri ripoti.
Ally amesema:”Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza jeraha lake alilofanyiwa upasuaji hatimae Hassan Dilunga kajiunga na kikosi kuanza mazoezi.
“Lengo la kumrudisha kikosini ni kuangalia utimamu wake wa kiafya ili timu yetu ya madaktari ijiridhishe kuwa yuko fiti kwa asilimia mia ngapi?
“Na pia Mwalimu Robertinho apate nafasi ya kumuangalia kiufundi ili atoe mapaendekezo yake. Mpaka sasa kila kitu kinaenda sawa tukisubiri ripoti ya mwisho ili uongozi ufanye maamuzi juu ya Hassan Dilunga.
“Tungefurahi kumuona kiungo wetu fundi akirejea kazini,”.