BEKI HUYU AINGIA ANGA ZA MSIMBAZI

NICKSON Kibabage nyota wa Singida Big Stars anatajwa kuwa katika rada za Simba.

Beki huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Hans Pluijm ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Ni mabao manne ametupia ndani ya ligi Kati ya 32 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya nne na pointi 51.

Akiwa ndani ya Singida Big Stars ni miongoni mwa nyota ambao walicheza Kombe la Mapinduzi pamoja na Kombe la Azam Sports Federation.

Katika Kombe la Azam Sports Federation wamegotea hatua ya nusu fainali waliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Liti ukisoma Singida Big Stars 0-1 Yanga.

Habari zimeeleza kuwa Simba ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi kwa sasa ikiwa ni upande wa ulinzi pamoja na ushambuliaji.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally hivi karibuni aliweka wazi kuwa mpango mkubwa kwenye usajili ni kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa.