MTIBWA SUGAR WAIVUTIA KASI POLISI TANZANIA

MTIBWA Sugar yenye maskani yake Morogoro kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo ni wa Ligi Kuu Bara ambao ni wa mzunguko wa pili.

Miongoni mwa mastaa ambao wapo kambini ni Razack Kimweri kipa anayekuzwa ndani ya chuo cha soka Bongo pale Morogoro, Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika Mei 15,2023.