MUDA HAUSUBIRI KAZI LAZIMA IENDELEE

MUDA hausubiri na kila mmoja anapambana kusaka ushindi kwenye mechi ambazo anacheza hilo ni jambo la muhimu kwa kila timu.

Wachezaji wanajituma na kufanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi na wapo ambao wamekuwa wakionyesha uwezo mkubwa ndani ya uwanja.

Kila timu ina kazi kusaka ushindi ikiwa ni kwenye mechi za lala salama kwa sasa kutokana na mechi kubakiwa chache za kucheza ambazo ni muhimu kupata ushindi.

Imekuwa kila mmoja kupambania kukamilisha hesabu ambazo zinapangwa na kila mmoja katika kutafuta matokeo uwanjani.

Pongezi kwa wale ambao wanatimiza majukumu yao kwenye mechi zao na wale ambao wapo kwenye maandalizi ya mechi za kukamilishia mzunguko wa pili ni muhimu kufanya kazi kubwa.

Ni ngumu kupata matokeo mazuri ikiwa hakutakuwa na maandalizi mazuri kwa kuwa kila timu inahitaji kupata ushindi na wachezaji wanajua kuwa timu ipo kwenye hatua gani.

Kila timu inatambua namna hali ilivyo na kupata matokeo ni muhimu kupata pointi hivyo ni muhimu kupambana katika kutafuta ushindi.

 Nidhamu inahitajika kwenye maandalizi ambayo kila mmoja anakwenda kufanya katika kutafuta ushindi kwa kuwa ni muhimu kuwa makini katika kutimiza majukumu.

Mashabiki nao wamekuwa wakijitokeza kwenye mechi nyingi uwanjani tangu mzunguko wa kwanza na sasa ni mzunguko wa pili hivyo wanastahili pongezi.

Kwa kazi kubwa ni muhimu kuendelea kuwa bega kwa bega na timu zao ili kuwaongezea nguvu wachezaji uwanjani.

Muda ambao umebaki kukamilisha mzunguko wa kwanza ni mfupi lakini inawezekana kukamilisha yote ambayo yapo na kila mmoja atapata kile anachostahili.

Kwa timu ambazo zipo Championnship kuna kupanda kama ilivyo kwa JKT Tanzania ambayo imeshajihakikishia nafasi yake msimu ujao ni muda wa kufanya maandalizi mazuri katika mechi zijazo.

Ukubwa wa kufanya kazi kwenye mechi za kukamilisha mzunguko wa pili ni muhimu kukamilisha mzunguko kwa umakini na inawezekana.

Wachezaji uwanjani kwenye lala salama mnapopewa nafasi ni muhimu kukamilisha na kuwapa burudani mashabiki wale ambao wanajitokeza kuona burudani.

Kila mmoja anapenda kufanya kazi nzuri kwenye ushindani wake na inawezekana ikiwa wataamua na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Muda ni huu na kazi nzuri kwenye miguu yenu inahitajika ili kutoa burudani ndani ya dakika 90 za ushindani ambazo zinafanyika.

Hakuna mechi nyepesi kutokana na kila timu kupambana kusaka ushindi kwenye hizo mechi na ni muda mzuri kukamilisha mahesabu.

Ukweli ni kwamba kila mchezaji anauwezo mkubwa kutokana na mechi husika na wachezaji wamekuwa wakifanya kazi kwa nyakati ambazo zipo.

Iwe hivyo kwenye mechi za mwisho na kila mmoja atimize majukumu yake kwa umakini ili kufanikisha malengo ya timu.

Kila la kheri kwenye majukumu ya wakati huu katika kukamilisha mzunguko wa pili.