Home Sports YANGA WAIVUTIA KASI SINGIDA BIG STARS

YANGA WAIVUTIA KASI SINGIDA BIG STARS

MENEJA wa Yanga, Walter Harrison ameweka wazi kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti, Mei 4,2023 ikiwa ni mzunguko wa pili.

Katika mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 4-1 Singida Big Stars.

Kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Mei 2 kilianza kufanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo.

“Kila kitu kipo sawa maandalizi yamekamilika na wachezaji wanatambua kuwa tunahitaji pointi tatu kikubwa ni kila mmoja kuona namna gani tunakwenda kuwakabili wapinzani wetu,”.

Previous articleSIMBA KAMILI KUIKABILI NAMUNGO
Next articleMKIA UNAPOKUWA MKUBWA KULIKO NG’OMBE