Home Sports SIMBA AKILI KWA NAMUNGO,YAIWEKA KANDO AZAM FC

SIMBA AKILI KWA NAMUNGO,YAIWEKA KANDO AZAM FC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni mchezo wao dhidi ya Namungo huku ule wa Azam FC ukiwekwa kiporo.

Mei 3 Simba inatarajiwa kumenyana na Namungo, Uwanja wa Majaliwa kwenye mchezo wa ligi na inakibarua cha kucheza na Azam FC,Mei 7 Uwanja wa Nangwanda, Sijaona.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanahitaji kupata matokeo kwenye mechi zote lakini wataanza na zile za ligi.

“Kwanza tuna mechi za ligi hapo unaona nguvu itakuwa kwenye mechi hizo kisha mchezo wetu dhidi ya Azam FC utafuata baadaye.

“Mchezo dhidi ya Azam FC upo karibu lakini hautakuwa mchezo wetu wa mwanzo kwa sasa hivyo ikifika wakati tutaanza maandalizi kwa mchezo huo hapo tutazungumzia kuhusu mchezo huo,” amesema Ally.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya  pili ikiwa na pointi 63 baada ya kucheza mechi 26.

Previous articleMKIA UNAPOKUWA MKUBWA KULIKO NG’OMBE
Next articleHIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA NAMUNGO