UBAO wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 0-0 Rivers United ikiwa ni mapumziko kwa sasa.
Huu ni mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali ambapo wawakilishi wa Tanzania wanapeperusha bendera.
Kwenye kipindi cha kwanza dakika ya 24 mchezo ulisimama kwa muda kutokana na tatizo la mwanga katika eneo la kuchezea kuwa hafifu na walipolishughulikia mchezo uliendelea.
Matokeo kwa sasa ni Yanga 2-0 Rivers kwa kuwa Yanga ilipata ushindi mchezo wa kwanza ugenini hivyo matokeo yakiwa hivi Yanga inatinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.