MANCHESTER United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ten Hag imesepa na pointi zote tatu muhimu dhidi ya Aston Villa.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford ubao umesoma Manchester United 1-0 Aston Villa.
Bao pekee la ushindi limefungwa na Bruno Fernandez dakika ya 39 kipindi cha kwanza na kuimaliza kazi mapema.
United inafikisha pointi 63 nafasi ya 4 huku Aston Villa nafasi ya 6 na pointi 54 kibindoni.
Vinara ni Manchester City wakiwa na pointi 76 baada ya kucheza mechi 32.