LICHA ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar, benchi la ufundi la Mbey City limebainisha kuwa bado kuna nafasi ya kubaki kwenye ligi.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Aprili 24 bao pekee la Kagera Sugar lilipachikwa kimiani na Ally Ramadhan, ‘Ufudu’ likamshinda kipa wa Mbeya City Haroun Mandanda ilikuwa dakika ya 88.
Timu hiyo imekusanya pointi 27 baada ya kucheza mechi 27 ipo kwenye hatari ya kushuka daraja.
Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema kuwa bado wana mechi za kucheza na watafanyia kazi makosa ambayo yametokea.
“Kweli matokeo ambayo tunapata sio mazuri lakini bado hatujakata tamaa kwa kuwa kuna mechi za kucheza hizo tatu zilizobaki tukipambana tukipata matokeo tutaondoka hapa tulipo.
“Hakuna ambaye anapenda kuona hatushindi ila ni mpira na haya ni matokeo kwenye uwanja wa mazoezi tunakwenda kufanyia kazi makosa, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.